Liverpool yawapiga bao Chelsea kwa kiungo mshambuliaji wa Shakhtar.

Alex Teixeira.
Katika wiki zilizopita ilionekana kuwa Chelsea ndio klabu pekee inayomfukuzia kiungo mshambuliaji wa kibrazil anayekipiga katika klabu ya Shakhtar Donetski aitwaye Alex teixeira, lakini alhamisi habari zilieleza kuwa klabu ya Liverpool ilipeleka dau la euro milioni 32 na ndio timu pekee iliyopeleka dau na inayopewa kipaumbele cha kumsajili kiungo huyo hatari katika dirisha hili dogo la usajili. Habari za karibu na klabu hiyo zinasema kuwa Chelsea iliacha mpango wa kumsajili mchezaji huyo kutokana na thamani kubwa waliyotajiwa huku wakiamini mchezaji huyo hana thamani hiyo, kutokana na hivyo basi kunaacha njia ikiwa nyeupe kwa Liverpool kumsajili mchezaji huyo ila pia gazeti la Times limeonya kuwa Liverpool wawe makini kufanya usajili huo haraka maana Chelsea huwa hawatabiriki maana waliwahi kuwanyang`anya Totenham Hotspur mchezaji waliyekuwa hatua za mwisho kumsajili ambaye leo ndiye Star wao wa timu (Willian).
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment