Mitandao yadai Giroud anaweza kukosa mechi ya leo kwa kuwa majeruhi.

Olivier Giroud.
Kuna taarifa zimesambaa mitandaoni kwa kasi hasa kwenye mtandao wa twitter zinazosema kuwa mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud amepata majeraha ya ankle wakati wa mazoezi ya mwisho na anaweza akakosa mchezo wa leo jioni dhidi ya Chelsea. Habari hizo zimetolewa na jamaa mmoja kwenye twitter anayetumia jina la  @DeanLDN22. Kitu kinachofanya watu wamwamini ni kuwa huyu jamaa wiki iliyopita ndiye aliyetoa taarifa za Mesut Ozil kukosa mechi ya Stoke, kwahiyo hatujui kama alibahatisha wiki iliyopita na hii ya ya leo ni uongo au anasema ukweli.


Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment