Old trafford hapatishi; Koeman.

Old Trafford.
Kocha mkuu wa klabu ya Southampton, Ronald Koeman amezungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mechi ya leo dhidi ya Manchester United hapo baadae itakayopigwa katika dimba maarufu duniani la Old trafford maarufu kama OT. Koeman amewahi kucheza katika uwanja huo kipindi cha nyuma na anasema ilikuwa ni vigumu sana kupata ushindi Old trafford kipindi hicho kuliko kipindi hichi  cha sasa ukizingatia kipindi hicho Manchester United walikuwa na wachezaji wanaopambania timu yao kuliko sasa hivi. Maneno hayo ya Koeman yanakuja baada ya msimu uliopita kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri katika uwanja huo walipopambana na Manchester United na ulikuwa ndio ushindi wa kwanza kwa Southampton kuupata baada ya miaka 27 kupita. Southampton wako nafasi ya 10 na wako nyuma kwa pointi 7 dhidi ya Manchester United baada ya mechi 22.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment