 |
Sanamu ya Cristiano Ronaldo iliyoharibiwa kwa rangi. |
Baada ya
Lionel Messi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia
(Balon d`or) kwa mara ya tano pale jijini
Zurich Uswizi na
Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili, kule kijijini kwa kina
Cristiano Ronaldo kwenye kisiwa cha
Madeira kulizuka watu wanaosadikika kuwa ni mashabiki wa mchezaji
Lionel Messi na wengine wakisema kuwa sio mashabiki wa
Lionel Messi bali ni wahuni wasiomkubali
Cristiano Ronaldo na waliipaka rangi mbalimbali huku wakiiandika jina la
Lionel Messi na namba
10 mgongoni ile sanamu ya
Cristiano Ronaldo iliyowekwa mwaka jana majira kama haya baada ya kushinda tuzo yake ya tatu ya
Balon d`or kwa mwaka 2014.
 |
Katia Aveiro, dada yake na Cristiano Ronaldo. |
Baada ya tukio hilo kutokea dada yake na
Cristiano Ronaldo aitwaye
Katia Aveiro alisema anasikitishwa sana na kitendo hicho na kusema kwamba roho imemuuma sana kwakuwa kaka yake hastahili utovu huo wa nidhamu kwa heshima aliyowaletea katika kisiwa hicho akipendacho cha
Madeira na kusisitiza kuwa wahuni hao wanafaa kwenda kuishi nchini
Syria maana wanafaa kukaa sehemu yenye vita kama hiyo huku akiomba msamaha kwa wote wanaoishi nchini
Syria akisema kuwa wapo ambao hawastahili kuishi kwenye mazingira hayo ila anaomba Mungu awaepushe na adha hiyo ya vita.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment