Mfahamu mchezaji bora wa FIFA ambaye Messi anamhofia kucheza nae.

Abdulaziz Alshehri
Abdulaziz Alshehri ni kijana wa miaka (25) akitokea katika nchi ya kiarabu ya Saudia Arabia na ndiye mchezaji namba moja kwa sasa wa gemu la FIFA duniani na alishinda tuzo hiyo ya  FIFA Interactive World Cup jijini Munich mnamo mwezi wa tano mwaka jana. Alshehri aliitumia Ureno katika mashindano hayo na alishinda na goli lake la ushindi alifunga Cristiano Ronaldo. Alshehri alizawadiwa $ 20,000 sawa na zaidi shilingi milioni 40 za kitanzania kwa kushinda mchezo huo. 
Abdulaziz Alshehri na Kaka wakicheza FIFA.
Abdulaziz Alshehri na Kaka.
Jumatatu Abdulaziz Alshehri alikua ni miongoni mwa wageni rasmi katika tuzo zenye heshima kubwa kwenye ulimwengu wa soka, maarufu kwa jina la Balon d`or na kabla ya kuanza kwa sherehe hiyo alipata bahati ya kukutana na mchezaji wa zamani wa dunia na timu ya taifa ya Brazil, maarufu kwa jina la Kaka na alifanikiwa kucheza nae gemu la FIFA na kufurahi pamoja.
Abdulaziz Alshehri akikabidhiwa tuzo na Cristiano Ronaldo.
Pia baadae alifanikiwa kukutana na magwiji wa soka wanaotamba kwa sasa duniani yaani Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar na alifanikiwa kupata tuzo ya heshima kutoka kwa Cristiano Ronaldo pamoja na kupata fursa ya kupiga picha mbalimbali na wakali hao wa kandanda ulimwenguni kwa sasa.
Abdulaziz Alshehri akiwa na mchezaji bora wa dunia Lionel Messi.
Abdulaziz Alshehri aliomba kucheza gemu la FIFA na wakali hao lakini waligoma huku Messi akisema hapana na Cristiano Ronaldo yeye alisema hawezi kucheza gemu hilo maana yeye hachezagi ila kwa maoni ya Abdulaziz Alshehri yeye alisema Messi anaogopa kupoteza mchezo huo akicheza nae maana anajua hawezi kushinda na Neymar ana mkataba na kampuni nyingine ya magemu ambayo haimruhusu kucheza gemu la FIFA
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment