(+VIDEO) Mascherano tumeshinda kwa sababu ya Messi.

Lionel Messi akiwatoka mabeki wa Malaga.
Beki wa kati wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Javier Mascherano ameelezea mchezo wa jana waliopiga na klabu ngumu ya Malaga na kufanikiwa kushinda bao mbili kwa moja. Mascherano anasema kitu pekee kilichowasaidia kushinda mchezo wa jana ni juhudi binafsi za mchezaji bora wa dunia Lionel Messi. Katika mechi hiyo iliyopigwa nyumbani kwa Malaga ilishuhudia klabu ya Barcelona ikihangaishwa muda wote wa mchezo japokuwa wao ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa kinda Munir El Haddad na baada ya dakika mbili Malaga walifanikiwa kurudisha bao hilo na kwenda mapumziko, lakini waliporudi Lionel Messi alifunga bao zuri akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na kiungo wa timu hiyo Ivan Rakitic na kufanya matokeo kuwa mbili kwa moja.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment