Barclays Premier League wazindua nembo mpya ya msimu ujao.

Nembo ya Premier League msimu ujao.
Ligi kuu nchini Uingereza maarufu kama Barclays Premier League hivi punde imezindua nembo mpya itakayotumika kwenye matangazo yote yahusuyo ligi hiyo huku ikiwa imewavutia wengi kwa namna ilivyosukwa upya. Nembo hiyo itaanza kutumika rasmi mwanzoni mwa msimu wa 2016/2017, Premier League imekuwa ikidhaminiwa na kampuni ya Barclays kwanzia msimu wa 2007/2008 na hii imekuwa mara ya kwanza kubadilishwa kwa nembo hiyo ndani ya muda wa miaka kumi. Maafisa wa Premier league wamekaririwa wakisema kuwa walitaka kuleta maneno ya udhamini mwingine ila wakaona waje kivingine, hiyo imetokana na udhamini walioupata wa zaidi ya paundi bilioni 5 kutoka kwenye matangazo ya television.

Richard Masters, Afisa mkuu wa Premier League.
Afisa mkuu wa Premier League bwana Richard Masters alikaririwa akisema kwanzia msimu ujao tutahama kutoka kwenye jina la udhamini tulilonalo sasa hivi na kuhamia kwenye Premier League tu, maamuzi haya yanatoa nafasi kwetu kujitambulisha kama chombo kinachojitegemea yaani (Organisation).

Hizi rangi zitakazotumika kwenye nembo ya Premier League msimu ujao.
Pia Premier League wamesema nembo hiyo itakuwa na uhusiano mkubwa na mashule na itakuwamo kwenye shule za msingi zipatazo 10,000 kwanzia mwanzo wa msimu ujao na wanategemea mpaka msimu wa 2021/2022 itakuwa imesambaa kwenye shule zote za msingi nchini humo.


Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment