 |
Alexis Sanchez. |
Kuna taarifa za kuaminika tumezipata hivi punde na tuna uhakika kuwa zitakuwa ni habari njema kwa mashabiki wa Arsenal. Taarifa hizo zinaeleza kuwa mazungumzo yaliyokwama hapo mwanzo kuhusiana na kuongeza mkataba wa nyota wa timu hiyo Alexis Sanchez yameanza tena na yanaendelea vizuri kiasi cha kutoa mwangaza wa nyota huyo klabuni hapo. Taarifa zinaeleza kuwa klabu ya Arsenal imejipanga kumpa Alexis mkataba wa miaka mitano na nusu ambao utamweka nyota huyo wa Chile klabuni hapo mpaka mwaka 2021 na atavuna kiasi cha paundi milioni 51.5 kutokana na mshahara wake. Sanchez alijiunga na Arsena mwaka 2014 akitokea kwa mabingwa wa ulaya FC Barcelona na amefanikiwa kufunga magoli 35 mpaka sasa.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment