Shabiki wa Arsenal afanya maamuzi magumu.
-Baada ya mechi ya jana baina ya Manchester United dhidi ya Arsenal kuisha kwa Arsenal kuambulia kipigo cha mabao matatu kwa mawili, Shabiki mmoja wa Arsenal huko London ameamua kuchana jezi yake sehemu ya mgongoni, sehemu ya moyo, sehemu ya tumboni na mikononi na akiwa tayari kuipiga bei kwa mtu anayeitaka. Maamuzi hayo yana maana kuwa Arsenal imekuwa timu isiyojiweza tena na bila shaka shabiki huyo hataki tena kuishabikia timu hiyo. Arsenal iko nyuma ya vinara wa ligi hiyo Leicester City kwa pointi 5.
0 comments:
Post a Comment