Kinda wa klabu ya Mancester United Marcus Rashford leo amekuwa nyota wa mchezo akiwa na umri mdogo wa miaka takribani kumi na nane kasoro. Rashford amewatandika Arsenal mabao mawili na kutengeneza moja, kinda huyo alianza kuwafunga Arsenal kupitia mpira wa krosi uliopigwa na kinda mwingine namba mbili aitwaye Varella haikupita mda kabla Rashford hajawaadhibu tena Arsenal kwa mpira wa kichwa na baadae kipindi cha pili alimtengenezea Ander Herrera bao zuri la tatu. Mabao ya Arsenal yalifungwa na Danny Welbeck pamoja na Mesut Ozil.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment