Arsenal na Spurs zafanya mabadiliko kuelekea London derby.

Mohamed Elneny.
Timu mahasimu wa jiji la London zinazokutana leo kwenye uwanja wa Whitehart Lane zimefanya mabadiliko ya vikosi vyao kuelekea mechi yao ya leo ambayo itaanza hivi punde. Arsenal wamefanya mabadiliko ya wachezaji wanne huku Spurs pia wakifanya hivyohivyo, Arsenal leo haitakuwa na wachezaji wake muhimu kama Petre Cech, Laurent Koscienly ambao wote hao ni majeruhi huku Olivier Giroud na Nacho Monreal wakianzia benchi na nafasi zao kuchukuliwa na Kieran Gibbs, Danny Welbeck, David Ospina na Mohamed Elneny atachukua nafasi ya Joel Campbel, Upande wa Spurs wachezaji wake muhimu watakuwa wamerudi uwanjani leo ambao ni Kyle Walker, Danny Rose, Musa Dembele na Dele Alli. Totenham wapo pointi tatu juu ya Arsenal.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment