Hazard anukia Madrid.

Eden Hazard.
Taarifa za ndani ya klabu ya Real Madrid zinaeleza kuwa upo mpango kabambe wa kuwapiga bei nyota wake ambao wameshindwa kuonyesha viwango vinavyostahili na fedha zitakazopatikana zitasaidia kuwanasa nyota mbalimbali wanaotakiwa na klabu hiyo na mmoja wa nyota wanaotakiwa kwa haraka ni Eden Hazard. Real Madrid imekuwa ikimfuatilia Hazard kwa muda mrefu bila mafanikio ila kwa mambo yanavyokwenda kwa sasa inaonekana Real Madrid haitapata wakati mgumu katika kumsajili nyota huyo kutokana na uhusiano wake na uongozi wa Chelsea kuporomoka kwa kiasi fulani. Madrid watakuwa tayari kuuza nyota wake wawili ili kupata fedha zaidi za kumnunua Hazard, nyota wanaotajwa kuwa sokoni ni Isco na James Rodriguez.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment