Hodgson asema Rooney atatakiwa kupambania namba.


Kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson ameongea na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya kikosi chake kuelekea mashindano ya Euro 2016. Hodgson amesema kuwa anajiamini na kikosi chake na anaamini kikosi hicho kitailetea England heshima kubwa hapo mwezi wa sita kwenye mashindano ya Euro, Pia Hodgson amegusia kuhusu ni nani atakuwa mshambuliaji wake namba moja haswa akizingatia kepteni wake Wayne Ronney amekuwa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha yake, na washambuliaji chipukizi wamekuwa hawana utani na nyavu, Roy amesema Rooney akirudi hakuna ubishi kuwa atatakiwa kupambana vya kutosha ili kupata namba kwenye kikosi hicho kilichosheheni washambuliaji hatari kama Jamie Vardy, Harry Kane na Danny Welbeck.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment