Ozil amtishia Wenger kwa Guardiola.
-Kiungo wa kijerumani anayechezea klabu ya Arsenal Mesut Ozil amemtaka kocha wake Arsen Wenger kusajili wachezaji wa kiwango cha juu maana msimu unaokuja utakuwa ni moja ya misimu migumu sana kwa ligi kuu ya Uingereza, Ozil amesema kama Wenger anataka kikosi chake kipambanie Ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu ujao ni lazima akiongezee nguvu ya kutosha maana kutakuwa na mtifuano wa hali ya juu ukizingatia ujio wa makocha wapya hususani Pep Guardiola, Ozil anasema Guardiola kila anapokwenda huwa anapata mafanikio kutokana na kujenga kikosi bora na anaamini atafanya hivyohivyo akiwa na Manchester City.
0 comments:
Post a Comment