Messi akataa kufananishwa na Cristiano.


Mchezaji bora wa dunia Lionel Messi amekataa kufananishwa na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Messi akiongea na waandishi wa habari alisema " Imekuwa ni tabia ya waandishi wa habari kwenye kila mkutano kuniuliza kuhusu mimi na Cristiano Ronaldo, Mimi sifanani na Cristiano Ronaldo wala mchezaji mwingine yeyote maana kila mtu ana ubora wake na malengo yake, mimi naangalia zaidi kuhusu kiwango changu na namna yakuisaidia timu yangu kushinda mataji" Messi aliongeza kwa kusema kuwa Real Madrid ni timu kubwa na imekuwa ikiwapa shida kila wanapokutana na anaamini mechi ijayo itakuwa ngumu pia. Barcelona watakutana na Real Madrid kwenye mchezo wa La liga unaojulikana kwa jina la El Classico.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment