 |
Anthony Martial. |
Katika tetesi mbalimbali za usajili siku ya leo katika mtandao wa
Le 10 sport wa nchini Ufaransa umedai kuwa mabingwa wa Ligue 1 Paris Saint Germain wameweka mipango thabiti ya kuhakikisha kuwa wanamng`oa nyota wa klabu ya Manchester United Anthony Martial. PSG wanamtaka Martial ili akazibe mapengo ya Zlatan Ibrahimovich na Edison Cavan kwa kuwa wanatarajiwa kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu. Inasemekana kuwa PSG hawatatumia nguvu nyingi kumshawishi Martial kwa kuwa wana wachezaji wengi wa kifaransa wanaocheza na Martial kwenye timu ya taifa na hao ndio watakaotumika kumshawishi Martial kujiunga na PSG.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment