Suarez ailazimisha Brazil.

Luis Suarez.
Mechi ya kufuzu kombe la dunia iliyopigwa majira ya saa 9 usiku kati ya Brazil na Uruguay imemalizika hivi punde na matokeo yamekuwa ni suluhu baada ya mshambuliaji wa FC Barcelona Luis Suarez kuisawazishia timu yake katika dakika ya 48 ya mchezo na kufanya matokeo kuwa ni mbili kwa mbili (2-2) mpaka mwisho wa mchezo. Brazil ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kwa winga wake anayekipiga katika klabu ya Bayer Munich Douglas Costa kabla ya Renato Augusto kuongeza bao la pili katika dakika ya 26 ya mchezo huku Edison Cavan akiifungia timu yake bao katika dakika ya 31 na katika dakika ya 48 Suarez alimalizia suluhu hiyo.


Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment