Giroud , Griezman na Matuidi waizamisha Uholanzi.


Mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Uholanzi iliyopigwa jana iliiisha kwa wenyeji kufungwa mabao matatu kwa mbili huku mechi hiyo ikitawaliwa na shukrani za dhati kutoka kwa mashabiki kwenda kwa mpenzi wao aliyewatoka juzi marehemu Johan Cruyff. Mashabiki wa pande zote mbili walionekana kubeba mabango mbalimbali yakionyesha kuhuzunishwa kwao na kifo cha Cruyff.
Moja ya mabango yaliyobebwa na mashabiki waliohudhuria mechi hiyo.

Ufaransa walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 6 kupitia kwa nyota wa Atletico Madrid Antonio Griezman kabla mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud hajaongeza bao la pili katika dakika ya 13 ya mchezo, Mabao hayo yalisawazishwa na Luke de jong kabla Ibrahim Affelay hajaongeza la pili katika dakika ya 86 lakini zilipita dakika mbili tu kabla Blaise Matuidi hajafunga bao la tatu na la ushindi katika dakika ya 88 na kufanya matokeo kuwa mabao matatu kwa mawili (2-3).




Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment