Mashabiki hawamtaki Wenger hata baada ya ushindi, Wenger awacharukia.

Bango linaloonyeshwa na mashabiki wa Arsenal kuwa ni mda wa Wenger kuwaachia timu yao.
Kwenye mechi ya jana ambayo klabu yake ya Arsenal ilishinda kwa mabao manne kwa sifuri dhidi ya Hull City, kuna baadhi ya mashabiki wa timu hiyo walikuwa wamebeba bango linalomshukuru Wenger kwa kumbukumbu nzuri alizoipa klabu hiyo lakini pia wakimtaka awaachie klabu yao maana wamemchoka. Wenger ambaye amekuwa hapo klabuni kwa miaka takribani 20 amewaeleza mashabiki hao kuwa hababaishwi na kelele zao maana ameshawazoea na rekodi yake kwenye klabu hiyo zinajieleza. Maneno hayo ya mashabiki wa Arsenal yamekuja baada ya timu hiyo kuonekana haitaweza tena kushinda taji la Epl kwa kuwa wameshaachwa na viongozi wa ligi hiyo kwa pointi nane.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment