Xavi amtaja mchezaji wa ligi ya Uingereza anayeweza kuichezea Barcelona.
-Kiungo wa zamani wa klabu ya FC Barcelona Xavi Hernandes, akiongea na waandishi wa habari wa Al Araby Al Jadeed jana alisema kuwa anaamini mchezaji wa klabu ya Leicester City na timu ya taifa ya Algeria Riyad Mahrez kuwa ana uwezo wa kuichezea klabu bora duniani Barcelona. Mahrez mpaka sasa ndiye mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza ikiwa amefunga mabao 16 na kutengeneza mengine 11 katika mechi 30 alizocheza msimu huu. Tayari Mahrez amehusishwa na uhamisho wa kwenda Barcelona na Xavi amebariki swala hilo.
0 comments:
Post a Comment