Ranieri ataja kikosi bora cha msimu.
-Kocha mkuu wa klabu ya Leicester City Claudio Ranieri ameongea na waandishi wa habari baada ya kupokea tuzo yake ya kocha bora wa mwezi na alikuwa na machache ya kuzungumza ambapo kati ya hayo aliulizwa na waandishi kuhusu ni wachezaji gani anaofikiri wanaweza kujenga kikosi cha msimu mpaka sasa na majibu yake yalikuwa yakushangaza na ya kufurahisha pia maana alisema haoni kama kuna tatizo wachezaji wake wote 11 wa Leicester City wakiunda kikosi hicho cha msimu maana wamefanya mambo yasiyokuwa yakawaida mpaka sasa. Riyad Mahrez na Wes Morgan ambao wote waliwekwa kwenye list ya mchezaji bora wa mwezi march wamejumuishwa sambamba na Jamie Vardy na N`Golo Kante kwenye kinyang`anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa msimu PFA. Hivyo basi kuna uwezekano Lecester City ikatoa zaidi ya wachezaji saba kwenye kikosi bora cha msimu.
0 comments:
Post a Comment