Totenham na Manchester City zamgombania mchezaji wa Arsenal.
-Klabu za Totenham Hotspur na Manchester City zimeripotiwa kuwa kwenye mbio za kuinasa saini ya aliyekuwa kepteni wa timu hiyo Mikel Arteta, Klabu hizo zinataka kumpa Arteta kazi ya ukocha ambayo amekuwa akijifunza kwa muda mrefu sasa na anaonekana kuimudu. Klabu ya Arsenal bado haijamuhakikishia Arteta kama itampa kibarua chochote cha kuinoa timu yao ya U21 au timu ya wakubwa. Arteta mwenye umri wa miaka 34 bado hajamaliza mkataba wake wa kuichezea Arsenal na hajaamua kama atastaafu soka ila kwa sasa klabu ya Manchester City inamuona kama msaidizi wa Pep Guardiola anayetarajiwa kutua klabuni hapo mwisho wa msimu huu.
0 comments:
Post a Comment