Perez asema kuna timu moja ndiyo itakayoamua ubingwa wa La Liga.


Mshambuliaji na mfungaji bora wa klabu ya Deportivo La Coruna Lucas Perez amesema baada ya Barcelona, Atletico Madrid na Real Madrid kuwa ndio wanaogombania ubingwa wa la liga basi Deportivo ndio watakaoamua nani achukue ubingwa huo kwa sababu watapambana na timu mbili kati ya hizo kwenye uwanja wao wa nyumbani. Perez anasema tutaamua nani achukue ubingwa, ninajua wengi mnasema ubingwa utaamuliwa May lakini sishangai maana wengi mlisema tayari bingwa anajulikana lakini mambo yamebadilika, ninajua Barcelona ni hatari wanapotafuta pointi na hata wasipotafuta, bado ni hatari lakini tutapambana nao. Deportivo wanacheza na Barcelona Alhamisi hii na pia watacheza na Real Madrid kwenye mchezo wa mwisho wa ligi mwezi wa tano.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment