Uwanja wa Anfield unaotumiwa na majogoo wa jiji la Liverpool jumanne iliyopita ulisimama kutoa heshima kwa mshambuliaji wa mashetani wekundu Manchester United Cristiano Ronaldo baada ya kuondokewa na mtoto wake wa kiume. Pia katika mchezo wa Jumamosi uwanja wa Emirates unaotumiwa na washika bunduki wa London klabu ya Arsenal ulitoa heshima kwa mchezaji huyu bora wa dunia mara tano. Hili ni tukio la kihistoria na kiungwana kwa wapenda soka wote duniani na limepongezwa na wapenzi wengi wa soka duniani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment