Arsenal yaitandika Newcastle United:

Olivier Giroud akifunga goli la kichwa dhidi ya Newcastle United.

Olivier Giroud akishangilia baadaya kufunga goli.

Klabu ya washika bunduki wa London wamefanikiwa kumtandika mbabe wa Chelsea klabu ya Newcastle kwa mabao (4-1) katika mchezo uliopigwa katika dimba la Emirates. Katika mchezo huo uliokua wa kusisimua kwa timu zote kushambuliana kwa kupokezana na kushtukiziana, Arsenal ndio waliofanikiwa kuongoza katika dakika ya (15) baada ya Olivier Giroud alipofunga bao safi la kichwa alipopokea krosi nzuri iliyotoka kwa Alexis Sanchez, bao hilo lilienda mpaka mapumziko, waliporudi katika dakika ya (54) Santiago Carzola aliyefikisha miaka 30 leo alifanikiwa kuiandikia timu yake bao la pili kabla Olivier Girioud kufunga bao la tatu akipokea krosi ya Hector Berellini katika dakika ya (58) zilipita dakika tano kabla ya mshambuliaji wa Newcastle Ayoze Perez kuipa timu yake bao la kwanza lakini haikutosha kuwanyamazisha washika bunduki na katika dakika ya (88) Santiago Carzola alifanikiwa kufunga bao la lake la pili katika mchezo na la nne kwa timu kwa mkwaju wa penalti baada ya Danieli Wellbeck kuchezewa rafu katika eneo la hatari na beki Dummet. Ushindi huo unaifanya Arsenal kufikisha pointi (26) sawa na Southampton wote wakiwa katika nafasi ya tano.

Uchambuzi wa viwango vya wachezaji:

Arsenal: Szczesny (6), Bellerin (8), Debuchy (7), Mertesacker (6), Gibbs (7), Flamini (6), Cazorla (8), Oxlade-Chamberlain (6), Sanchez (8), Welbeck (7), Giroud (8)
Subs: Podolski (6), Coquelin (6), Maitland-Niles (6)
Newcastle: Alnwick (6), Janmaat (6), Williamson (6), Coloccini (5), Dummett (4), Tiote (5), Colback (5), Gouffran (5), Perez (6), Ameobi (6), Cisse (5)
Subs: Riviere (6), Cabella (6), Armstrong (6).
Man of the Match: Oliver Giroud
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment