Lampard aipaisha Man city:

Frank Lampard akishangilia baada ya kufunga bao pekee katika mchezo dhidi ya Leicester City.

Frank Lampard leo ameweza kuipaisha klabu yake anayoichezea kwa mkopo Manchester City kwa kuipa ushindi wa bao(1-0) ugenini dhidi ya timu ngumu iliyopanda daraja msimu huu Leicester City. Katika mechi hiyo Frank alifanikiwa kufunga bao lake la (175) katika ligi ya uingereza na kumfanya kua sawa na gwiji wa Arsenal (Thiery Henry). Mbali na ushindi huo klabu ya Man city imezidi kupata majeruhi kufuatia kuumia kwa mshambuliaji Eden Dzeko wakati akipasha misuli moto kabla ya kuanza kwa mechi, pia Vicent Company naye amepata majeraha yaliyomsababisha kushindwa kuendelea na mechi. Kwa ushindi huo Man City wamefanikiwa kufikisha pointi (36) nyuma ya vinara Chelsea.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment