UEFA MTOANO, PSG MDOMONI KWA CHELSEA HUKU MAN CITY MDOMONI KWA FC BARCELONA.

UEFA RAUNDI YA KUMI NA SITA BORA:

Manchester city versus FC Barcelona, Schalke 04 versus Real Madrid.

Mabingwa watetezi Klabu ya Real Madrid walioko huko Morocco wakicheza kombe la klabu bingwa ya dunia wenyewe katika raundi ya kumi na sita bora watakutana na klabu ya Schalke 04 ya huko Ujerumani wakati mahasimu wao FC Barcelona watakapo kwaana na mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Manchester City na ikiwa ni mara yao ya pili mfululizo kukutana wakati Man City wakikumbuka kichapo walichopokea kutoka kwa wacatalunya hao msimu uliopita.

Paris Saint Germain versus Chelsea Football Club

Klabu ya Paris Saint Germain wamepewa nafasi ya kulipiza kisasi kwa klabu ya matajiri wa london Chelsea, ikiwa ni mara yao ya pili mfululizo kukutana na PSG ikikumbuka kichapo ilichopokea pale Stamford Bridge. Itakua ni mechi ya kuvutia zaidi ikizingatiwa kwamba klabu zote zina wachezaji mahiri kama Zlatan Ibrahimovich (Ibracadabra), Eden Hazard, Edison Cavan, Diego Costa na wengine wengi.

Shakhtar Donetski versus FC Bayern Munich, Bayern Leverkusen versus Atletico Madrid.

Mabingwa wa huko Ujerumani klabu ya Bayern Munich wenyewe watakutana na klabu ngumu ya huko Ukraine ambayo inafahamika kwa jina la Shakhtar Donestik, huku majirani zao Bayern Leverkruzen wakikutana na na mabingwa wa ligi ya Hispania klabu ya Atletico de Madrid hawa wanakumbukwa kwa kufika hatua ya fainali katika mashindano yaliyopita.

Juventus versus Borrusia Dortmund.

Borrusia Dortmund wao wanakutana na vizee vya Turin, mabingwa wa Italia klabu ya Juventus hii itakua ni moja ya mechi nzuri sana ikizingatiwa kwamba Borussia hawana mcheza kwenye UEFA pia na Juventus wakiamini kwamba ni zamu yao ya kunyakua ubingwa wa ulaya kwani wana kikosi bora na kilichokamilika.

Arsenal FC versus AS Monaco, FC Basel versus FC Porto.

Klabu ya Arsenal wao safari hii wamekutana angalau na timu ambayo wanaweza kupambana nayo na sidhani kama watakua na la kulalamikia, washika bunduki watakutana na Mabingwa wa kombe la Emirates Fc Monaco ya huko Ufaransa. Fc Porto watakutana na timu iliyotoka kundi gumu kabisa klabu ya FC Basel, ikumbukwe pia klabu ya FC Porto ni moja ya klabu tatu ambazo hazijafungwa katika hatua ya makundi, timu nyingine mbili ni Real Madrid na Chelsea ambazo zote hazikufungwa.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 comments: