 |
FC Barcelona wakipongezana baada ya kuikandamiza SD Huesca bao 8-1. |
.jpg) |
Pedro akishangilia baada ya kupiga bao. |
Klabu ya FC Barcelona usiku wa kuamkia leo wamefanya mauaji ya kutisha kwa timu ya SD Huesca kwa kuipiga bao nane kwa moja (8-1) kwenye uwanja wao wa Nou Camp katika mashindano ya Copa del Rey, Mabao ya Barcelona yalianza kufungwa na Pedro Rodriguez katika dakika ya (20) na (26) kabla ya Sergi Roberto kuipatia barca bao la tatu katika dakika ya (29) zilipita dakika kumi tu kabla Andres Iniesta hajaiandikia timu yake bao la nne katika dakika ya (39) na kabla ya kwenda mapumziko Pedro alimaliza kazi yake kwa kupiga bao la tatu katika dakika ya (43). Waliporudi kutoka mapumziko Adriano Correia aliipatia timu yake bao la sita katika dakika ya (68) na zilipita dakika kumi tu kabla Adama Traore hajaiandikia timu yake bao la saba katika dakika ya (78) na katika dakika ya (83) Sandro Ramirez alimalizia karamu hiyo ya magoli nane, nao SD Huesca walipata bao lao la kufutia machozi katika dakika ya (86) ya mchezo kupitia kwa Carlos Moreno.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment