![]() |
Andre Schurrle, Eden Hazard na Azpillcueta wakipongezana baada ya kufanya vizuri. |
Eden Hazard jana alifanikiwa kuipaisha timu yake kwenye mchezo wa kombe la ligi baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa magoli matatu kwa moja (1-3) ugenini dhidi ya Derby County, mabao ya Chelsea yalifungwa na Eden Hazard katika dakika ya (23) ya mchezo na bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha pili ambapo mchezaji aliyetokea benchi Fellipe Luiz alipoongeza bao la pili katika dakika ya (56) na katika dakika ya (71) Derby County walijipatia bao kupitia kwa C. Bryson lakini halikutosha kuwanyamazisha (Blues) kwani katika dakika ya (82) Mjerumani Andre Schurrle alimaliza kazi baada ya kupiga bao la tatu na la mwisho katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa iPro Stadium, Derby na kuhudhuriwa na mashabiki 30639.
0 comments:
Post a Comment