THIERRY HENRY ATANGAZA KUSTAAFU SOKA.

Thierry Henry akishangilia kombe la dunia 1998 walipoifunga Brazil.

Mkongwe wa zamani wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa (Les blues) Thierry Henry (37) ametangaza kustaafu kucheza soka baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya New York Redbulls. Thierry Henry ametangaza uamuzi huo muda mfupi uliopita kwa kusema yafuatayo


Thierry Henry
Siku Thierry Henry aliposajiliwa na Arsen Wenger.

"Baada ya miaka 20 katika mchezo wa soka nimeamua kustaafu kucheza soka la kulipwa na imekua ni safari nzuri sana na ya ajabu katika maisha yangu, ninapenda kuwashukuru mashabiki, wachezaji wenzangu  na mtu mmoja mmoja kwa ujumla haswa katika kipindi changu nilipokua Monaco, Juventus, Arsenal, Barcelona na New York Redbulls na heshima za pekee kwa timu yangu ya taifa kwa kuifanya safari yangu kuwa ya kipekee".Pia katika website yake mshindi huyu wa kombe la dunia mwaka 1998 alidokeza machache yafuatayo;

Thierry Henry akishangilia.

"Ni muda mwingine tena wa kuelekea katika mwelekeo mwingine wa maisha, ninayo heshima kuwaeleza kua ninaelekea kurudi LONDON ambako nitajiunga na SKY SPORTS katika kuchangia mawazo na mapendekezo na uzoefu niliojifunza nanyi kwa kipindi chote."

"Nimekua na kumbukumbu za ajabu na nyingi zikiwa nzuri na uzoefu wa ajabu pia. Ni matumaini yangu mmefurahia soka langu nililocheza kama mimi nilivyofurahi kucheza soka. Tukutane upande mwingine (See you on the other side)".

Hayo ni maneno aliyoyaandika gwiji la soka Thierry Henry katika mtandao wake binafsi. Ikumbukwe pia Thierry Henry alianza kucheza soka akiwa na klabu ya Monaco kabla ya muda mfupi kujiunga na Juventus na ilipofika mwezi wa nane (8) 1999 alijiunga na klabu ya Arsenal.

Henry akishangilia baada ya kuifunga Real Madrid kwenye UEFA

Mshambuliaji huyu hatari alikuja kuwa hatari katika ligi ya uingereza baada ya kuifungia klabu yake ya Arsenal zaidi ya magoli 200 na alifanikiwa kushinda mataji mawili ya Barclays Premier league pamoja na makombe matatu ya FA.

Baada ya kufanikiwa sana akiwa na Arsenal alihamia katika klabu ya FC Barcelona na kucheza katika ligi ya hispania La Liga na kufanikiwa kushinda mataji kibao kama La Liga, Copa del Rey, Champions League, Club World Cup, Spanish Super Cup na European Super Cup katika mwaka wa 2009.
Thierry Henry akishangili na kombe la UEFA baada ya kuwashinda Manchester United 2009 pale ROMA.


Thierry Henry amemalizia soka lake katika klabu ya New York Redbulls katika ligi ya MLS Marekani.


Thierry Henry

Thierry Henry
Kwa ujumla Thierry Henry amefanikiwa kufunga magoli 51 katika michezo 123 akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa na kushinda kombe la dunia mwaka 1998 na lile la Euro mwaka 2000.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment