REAL MADRID YAINGIA FAINALI YA KLABU BINGWA YA DUNIA KWA KISHINDO.

Sergio Ramos akishangili baada ya kufunga goli.

Cristiano Ronaldo 
Klabu bingwa wa ulaya (UEFA) Real Madrid imeendeleza wimbi lake la ushindi wa (21) mfululizo katika mashindano ya klabu bingwa ya dunia huko Morocco baada ya kuichapa timu ya Cruz Azul ya Mexico kwa mabao manne kwa sifuri (4-0), mabao ya Real Madrid yalifungwa na Sergio Ramos katika dakika ya (15), Karim Benzema (36), Gareth Bale (50) na kijana mdogo wa kihispaniola Isco alihitimisha karamu hiyo baada ya kutengenezewa pande safi na mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo katika dakika ya (72) na kufanaya matokeo kuwa, Cruz Azul 0-4 Real Madrid. Mabingwa hawa wa ulaya ambao walipata ushangiliaji wa aina yake kutoka kwa mashabiki wa Morocco watacheza fainali hapo jumamosi na timu mojawapo kati ya Auckland City au San Lorenzo amabazo zinacheza leo mechi yao ya nusu fainali.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment