KOMBE LA LIGI NUSU FAINALI NI LIVERPOOL DHIDI YA CHELSEA.



Liverpool wakishangilia bao.
Lazar Markovich

Kombe la ligi huko Uingereza liliendelea jana kwa majogoo wa jiji Liverpool kushinda ugenini dhidi ya Bournemouth. Liverpool wamefanikiwa kuamka kutoka usingizini baada ya mwisho wa wiki kukubali kichapo cha bao tatu kutoka kwa mahasimu wao Manchester United, jana vijana wa Brendan Rodgers walifanikiwa kuishinda Bournemouth kwa bao tatu kwa bila (0-3), mabao ya Liverpool yalifungwa na Raheem Sterling mawili (2) na Lazar Markovich aliyefunga bao lake la kwanza tangu asajiliwe katika timu hiyo ya jiji la Merseyside. Kwa ushindi huo Liverpool itakwaana na vigogo wa ligi kuu ambao ni Chelsea katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa katika uwanja wa nyumbani wa Liverpool Anfield.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment