ROBERTO CARLOS ASEMA CRISTIANO RONALDO NI MOTO KULIKO MESSI:

Roberto Carlos.
Roberto Carlos anaamini kuwa Cristiano Ronaldo ni moto wa kuotea mbali kuliko staa wa FC Barcelona Lionel Messi.

Beki huyu wa kushoto wa Brazil na Real Madrid mwenye miaka (41) sasa alifanikiwa kuichezea timu ya Real Madrid michezo (527) kati ya mwaka (1996-2007) ameonyesha kukoshwa na kiwango cha staa huyo wa timu yake ya zamani na kusema anaamini Cristiano Ronaldo ni bora kuliko Muargentina Lionel Messi.

Cristiano Ronaldo

Lionel Messi

Roberto Carlos alikaririwa akisema haya "Cristiano Ronaldo anabakia kua mchezaji bora wa dunia na Messi anaendelea kufanya vitu ambavyo watu wengine wameshindwa kuvifanya (Cristiano Ronaldo remains the best in the world, and Messi is doing what others have failed to do)", Pia aliuambia mtandao wa Onda Cero kuwa "Messi anavunja rekodi lakini Ronaldo ni mchezaji mwenye maamuzi makubwa au lugha nyingine ni mchezaji aliyekamilika kuliko Messi ( He is breaking records, but Cristiano is more decisive than him)".
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment