 |
Wayne Rooney |
 |
David de Gea |
Baada ya mwisho wa wiki kuwashughulikia vizuri mahasimu wao maarufu kwa jina la majogoo wa jiji (Liverpool) kwa kuwapiga bao 3-0, kepteni wa mashetani wekundu (Manchester United) Wayne Rooney amepata nguvu ya kueleza wazi kwamba sasa wako fiti na wamerudi kwenye kinyang`anyiro cha ubingwa tena bila woga wowote amesema anaamini wana uwezo wa kunyakua ubingwa huo dhidi ya Chelsea na majirani zao Manchester City kwa sababu hapo mwanzo waliachwa pointi nyingi na sasa wamebakiza pointi nane tu kuwafikia viongozi wa ligi hiyo ambao ni Chelsea. Manchester United kwa sasa wanashikilia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi baada ya kushinda michezo takribani 6 mfululizo na wakiwa na pointi 31 baada ya kucheza michezo 16. Pia Rooney amemsifia kipa wake mhispaniola David De Gea na kusema kuwa kipa huyo ni moja ya makipa bora wa dunia, aliyasema hayo kufuatia kiwango De Gea alichokionyesha dhidi ya Liverpool.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment