SD Huesca yachapwa bao nne kwa bila na FC Barcelona (0-4) katika raundi ya kumi na sita ya kombe la mfalme (Copa del` rey).


Rakitic

Klabu ya Fc Barcelona jana walifanikiwa kuichapa timu ya SD Huesca bao nne kwa nunge. Barcelona waliandika bao lao la kwanza katika dakika ya (16) kupitia kwa kiungo wao waliyemsajili kutoka sevilla, Ivan Rakitic aliyepiga faul nzuri iliyotinga wavuni bila bugudha, zilipita dakika nne tu kabla ya Andres Iniesta (fundi) kuiandikia Barcelona bao la pili na la kwaza kwake kwa msimu huu. Katika dakika ya (38) Iniesta alimtafunia Pedro Rodriguez pande maridadi na kusababisha Pedro kuwaandikia wacatalunya bao la tatu, haikuishia hapo bali katika dakika ya (71) nduguye Thiago Alcantara, huyu si mwingine ni Rafinha Alcantara alihitimisha karamu ya magoli manne kwa bila.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment