Wenger aahidi kusajili mmoja Arsenal.

Arsene Wenger
Kocha mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger jana kabla ya mechi kati yao na timu ngumu ya Stoke City, Wenger aliwaeleza waandishi wa habari kwamba anaweza kuongeza beki mmoja katika dirisha dogo la usajili na akasisitiza kuwa mashabiki wa timu hiyo wanapaswa kuwa wavumilivu kwani kuna klabu kubwa ambazo ziko sokoni pia zikisaka wachezaji kwa fedha nyingi kitu ambacho yeye hawezi kufanya. Katika mechi ya jana pia Wenger ameendelea kupoteza beki mwingine baada ya Mathieu Debuchy kuumia bega na atahitaji kufanyiwa upasuaji mapema iwezekanavyo kwa hiyo Wenger atalazimika kuingia sokoni kusaka beki mzoefu namba 2 wa kuziba pengo hilo.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment