Hapo baadae wapenzi wa soka duniani kote wataelekeza macho yao na masikio huko Zurich ambako kutakua na shughuli za kuwatangaza nguli wa mchezo wa soka duniani waliofanya vizuri kwa mwaka 2014, katika shughuli hiyo atakuwamo rais wa FIFA, Sepp Blatter akiwa kama mgeni rasmi wa shughuli hiyo sambamba na viongozi wengine wa taasisi hiyo kubwa ya soka duniani kama Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele na wengine wengi watakao kuwa wakikabidhi zawadi kwa washindi.
Katika shughuli hiyo kutatangazwa mchezaji bora wa mwaka 2014, na katika safu hiyo watapambana wachezaji watatu bora kabisa waliokwisha pendekezwa na wawili kati yao wamekwisha zoeleka kuwamo katika tatu bora ambao ni mshindi wa mwaka jana Cristiano Ronaldo na ndiye anayeonekana kuwa bora kuliko wenzake wa pili ni mshindi wa tuzo hiyo kwa mara nne mfululizo huyu si mwingine bali ni Muargentina Lionel Messi, huyu pia ana nafasi ya kushinda tuzo hii kwa mara ya tano ila yeye hakufanikiwa kuisaidia timu yake ya FC Barcelona kunyakua kombe lolote wala timu yake ya taifa kunyakua kombe lolote, na wa mwisho anakuwa ni kipa bora wa dunia kwa mwaka 2014 huyu si mwingine ni Manuel Neuer, huyu ni mmoja kati ya makipa wachache waliowahi kutokea katika ulimwengu wa soka na kuweza kuingia katika kinyang`anyiro hichi na pia huyu jamaa amekuwa na msimu mzuri katika klabu yake kwa kuisaidia kupata ubingwa wa Bundesliga na timu ya taifa kuipa Ubingwa wa dunia, anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hii.
Katika kipengele cha pili kutakuwa na kinyang`anyiro cha kocha bora wa mwaka na katika kinyang`anyiro hicho wamo makocha waliofanya vizuri katika mwaka wa 2014, wa kwanza anakuwa ni Joachim Low, huyu ni kocha wa mabingwa wa dunia Ujerumani, wa pili ni kocha wa klabu bingwa ya ulaya na dunia (Real Madrid) Carlo Ancelloti na wa mwisho ni kocha wa mabingwa wa ligi ya Hispania maarufu kama La liga hawa si wengine ni Atletico Madrid na kocha wao ni Diego Simeone, huyu anakamilisha makocha wa tatu watakao menyana katika kipengele hicho kwa mwaka 2014.
Katika kipengele cha tatu kutakua na kutangazwa kwa kikosi bora cha mwaka 2014, mbali na kutangazwa kwa wachezaji hao, pia kutakua na kutangazwa kwa goli bora la mwaka 2014 (puskas) na katika kinyang`anyiro hicho wamo wachezaji watatu waliofunga magoli ya kushangaza, katika orodha hiyo yumo Robin Van Persie dhidi ya Hispania katika kombe la dunia, James Rodriguez dhidi ya Uruguay na mwanadada Stephanie Roche dhidi ya Wexford Youths, hawa wote walitingisha nyavu kwa magoli ya aina yake.
Pia kutakua na kinyang`anyiro cha mchezaji bora wa kike wa mwaka 2014 kitakachowakutanisha wachezaji bora kabisa kama wafuatavyo: Nadine Kessler wa Ujerumani, Marta wa Brazil na Abby Wambach wa Marekani.
Tafrija hiyo inatazamiwa kufanyika mida ya jioni kwa huku Afrika ya Mashariki na kama kawaida yake itafanyika huko mjini Zurich, Uswisi leo.
0 comments:
Post a Comment