Messi aiweka Barca kikaangoni tena.


Baada ya mchezo wa jana, star wa timu ya FC Barcelona Lionel Messi alikanusha habari zote za yeye kuhama katika klabu hiyo ambayo imemlea tangu akiwa mdogo na kufanikiwa kuwa mfungaji wa klabu hiyo wa muda wote na mfungaji bora wa la liga, Messi alikaririwa akisema "kuwa taarifa za yeye kuhamia Chelsea au M anchester City ni za uongo" na hana mpango wowote wa kuhama Barcelona lakini hivi punde akiwa kule Uswisi katika jiji la Zurich, Messi akiwa na wenzake wawili yaani Cristiano Ronaldo na Manuel Neuer walikua wakijibu maswali mbalimbali na swali moja aliulizwa Messi ni kwamba mwakani unategemea kuwa na timu gani mwakani? Messi akajibu akasema sijui mwakani nitakua na klabu gani, Hiyo ni kauli aliyoitoa Lionel Messi hivi punde na ni kauli inayopingana na kauli yake ya jana na pia ni kauli inayowaweka mashabiki wengi wa Barcelona katika maswali yasiyo na majibu juu ya staa wao huyo.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment