 |
Kelechi Nwakali na Samweli Chukwueze. |
Kocha mkuu wa Arsenal, Arsen Wenger amefanya usajili mwingine majira haya ya dirisha dogo la usajili na amezidi kuwafurahisha mashabiki wote barani Afrika baada ya kusajili vijana wawili wenye vipaji vya hali ya juu kutoka nchini Nigeria. Wenger amesajili vijana hao baada ya kuwasiliana na wakala wake nchini Nigeria ambaye alikuwa mchezaji wake wa zamani Nwanko Kanu na amefikia makubaliano ya kuwasajili vijana hao leo majira ya asubuhi. Vijana hao ni kapteni wa timu ya U17 Kelechi Nwakali na mwenzake Samweli Chukwueze, pia ikumbukwe kuwa vijana hawa ni wale walioiletea Nigeria na Afrika heshima kubwa baada ya kushinda kombe la dunia la U17. Wenger amekuwa akiwaamini wachezaji kutoka Afrika na haswa Nigeria na wamekuwa wakifanya vizuri sana kama Alex Iwobi aliyesajili majira ya joto yaliyopita ameshadhihirisha ubora wake kuonyesha kiwango cha hali ya juu na kumfanya Arsen Wenger kumuamini sana.

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment