Welbeck arudi Arsenal.

Danny Welbeck.
Taarifa za ndani za klabu ya Arsenal leo mapema zimeripoti kuwa mshambuliaji wake mahiri raia wa Uingereza Danny Welbeck amerudi uwanjani baada ya kukaa nje kwa muda mrefu. Danny Welbeck amekuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi tisa, mechi ya mwisho ya Danny ilikuwa dhidi ya mahasimu wao Chelsea iliyopigwa katika uwanja wa Emirates mwezi wa nne na ilimalizika kwa sare ya bila kufungana. Danny Welbeck atajumuishwa kwenye kikosi cha kwanza baadae mwezi ujao ila kwa sasa anatarajiwa kucheza mechi za U21 haswa mechi itakayopigwa mwezi wa pili dhidi ya Brighton.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment