Arsenal inamfukuzia mshambuliaji hatari wa Nigeria.

Odion.
Klabu ya Arsenal inaripotiwa kuwa katika mbio za kuinasa saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria na klabu ya Watford ya England, mshambuliaji huyo anayefahamika kwa jina la Odion Ighalo anakipiga katika klabu ya Watford na amekuwa mhimili mkubwa katika timu hiyo haswa katika mechi kubwa za ligi kuu ya Uingereza. Taarifa zinaeleza kuwa Ighalo atakuwa njiani kuondoka katika klabu hiyo kutokana kwamba klabu ya Watford imeanza kumfukuzia mshambuliaji wa klabu ya Granada nchini Hispania aitwaye Isaac Success (20), Success amefunga jumla ya mabao manne msimu huu huku Ighalo akifunga mabao 15 ya ligi mpaka sasa.

Isaac Success.

Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment