 |
Cicinho na Zidane. |
Beki wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil amemwelezea mchezaji mwenzake wa zamani wa Real Madrid na sasa kocha Zinedine Zidane kuwa ni mtu sahihi katika klabu hiyo na muda si mrefu ataifanya timu hiyo kucheza soka safi kama linalochezwa na FC Barcelona. Cicinho anasema kuwa Zidane apewe muda kidogo tu na ataifanya timu hiyo kuwa moja ya timu zinazocheza soka la kuvutia duniani. Sababu zinazomfanya Cicinho kuamini Zidane ataifanya klabu hiyo kucheza soka safi ni kuwa na wachezaji wazuri haswa washambuliaji na viungo na anasema hata kama Madrid ikifungwa mabao mawili au matatu, wenyewe hufunga zaidi ya mabao matano kwaiyo ni jambo zuri kama klabu ina wafungaji mahiri.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment