Carlo Anceloti atabiri mechi ya Chelsea na PSG.

Carlo Ancelotti.
Kocha mwenye jina kubwa duniani Carlo Anceloti ambaye pia amewahi kuwa kocha wa timu zote mbili yaani Chelsea na Paris Saint Germain, zinazokutana leo kwenye ligi ya mabingwa maarufu kama UEFA, Ancelotti ametoa utabiri wake kuhusiana na mechi hiyo kali itakayopigwa kwenye uwanja wa Parc de France, akiongea na mwandishi mmoja wa mtandao wa Goal.com Ancelotti alisema kuwa Chelsea itacheza kwa kuzuia zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza huku PSG wakicheza mpira mwingi huku wakitafuta ushindi utakaowapa nafuu watakapoenda Stamford Bridge, Pia Ancelotti anasema PSG watapata wakati mgumu kutokana na Chelsea kuwa na kocha Guus Hiddink ambaye anaifanya timu hiyo kucheza kwa ustadi mkubwa wa kuturuhusu kufungwa. Chelsea wamesafiri bila ya kepteni wao John Terry na Kurt Zuma kutokana na majeraha waliyonayo.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment