Ronaldo awatemea cheche waandishi wa habari.

Cristiano Ronaldo.
Mshambuliaji bora wa klabu ya Real Madrid na pia mshindi wa tuzo ya Ballon d`or mara tatu Cristiano Ronaldo, amezungumza na waandishi wa habari mjini Roma kuelekea kwenye mechi yao ya klabu bingwa ulaya dhidi ya As Roma na waandishi wa habari walikuwa na machache ya kumuuliza kama kuhusiana na penalti iliyopigwa juzi na mpinzani wake mkubwa kisoka Lionel Messi, Ronaldo alijibu akisema ninajua kwanini Messi alimpasia Suarez na hakutaka kufafanua zaidi kuhusiana na suala hilo, Swali la pili aliulizwa juu ya urafiki wake na Gareth Bale, alijibu akisema sio lazima kuwa na marafiki ndani ya timu unayocheza, mbona mwaka 2008 wakati tunachukua UEFA na Manchester United sikuwa nikiongea sana na wakina Giggs, Scholes na Rio Ferdinand, Pia swali la tatu lilikuwa likimuhusu yeye kwanini hafungi magoli kwenye mechi za ugenini ndipo alipowauliza swali waandishi wa habari kuwa wamtajie ni nani amefunga magoli mengi ya ugenini kuliko yeye tangu ametua Hispania? Waandishi hawakuweza kumjibu ndipo akaamua kunyanyuka na kuondoka zake.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment