(+Video) Penati ya Messi na Suarez yazua utata.

Luis Suarez akishangilia bao na Lionel Messi.
Katika mchezo wa La Liga uliopigwa jana katika dimba la Nou Camp kati ya FC Barcelona na Celta Vigo, wachezaji wa Barcelona Lionel Messi na Luis Suarez walifanya tendo la ajabu ambalo halijazoeleka kwenye ulimwengu wa soka. Wakati FC Barcelona wakiwa wanaongoza kwa mabao matatu kwa moja, walipata penalti ambayo alienda kuipiga mchezaji bora wa dunia Lionel Messi, wakati Messi anaipiga alitoa pasi kwa Luis Suarez badala ya kuipiga moja kwa moja na kitendo hicho kimekua gumzo leo karibia kwenye mitandao yote ya kijamii baadhi ya watu wakishangaa inakuaje bao hilo likawa halali na wengine wakisema ni halali kama refa alivyoamua iwe. Bao kama hilo pia amewahi kufunga gwiji wa klabu ya Barcelona Johan Cruyf akiwa na Olsen.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment