 |
Petre Cech. |
Kipa mahiri wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Czech Republic ameeleza sababu ya wao kufungwa kwenye ligi ya mabingwa ulaya na FC Barcelona kwenye mechi ya jana. Cech akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mechi hiyo alisema kuwa kukosa umakini kwenye kufunga magoli ndiko kuliwapa Barcelona nguvu ya kushinda ila kama wangetumia vizuri nafasi walizopata basi mambo yangekuwa mengine, Pia amesisitiza kuwa hajisikii vibaya kufungwa na Messi ila anajisikia vibaya kwa kupoteza mechi muhimu kama ile. Barcelona waliifunga Arsenal mabao mawili kwa bila na yote yaliwekwa kimiani na mshambuliaji hatari na bora zaidi duniani Lionel Messi.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment