 |
John Terry. |
Klabu ya Chelsea leo imetoa taarifa kadhaa kuhusiana na wachezaji wake ambao ni majeruhi wa muda mfupi. Kuelekea kwenye mechi yao ya kombe la FA dhidi ya Manchester City kocha wa timu hiyo Guus Hiddink akiongea na waandishi wa habari alieleza kuwa hakuna majeruhi waliongezeka mpaka sasa cha zaidi ni kwamba John Terry bado hatakuwa fiti kucheza mchezo huo na itabidi ukuta wa timu hiyo ubaki kama ulivyocheza na PSG kwenye klabu bingwa ulaya, Pia mchezaji wa kibrazil waliyemsajili kutoka timu ya Corinthians katika dirisha dogo la usajili Alexandre Pato bado hayuko fiti kuanza kucheza kwa sasa.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment