Manchester United yasubiria mechi hii kumfukuza Van Gaal.

Louis Van Gaal.
Taarifa za ndani ya klabu ya Manchester United zinadai kuwa tayari familia ya Glazer imemweleza mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo bwana Edwood kuwa afanye analoweza kuiokoa timu kutoka kwenye matokeo mabovu wanayoyapata hivi karibuni hata ikibidi kumfukuza kocha wa timu hiyo kabla msimu haujakwisha, familia ya Glazer imeamua kumfungukia bwana Edwood haswa baada ya timu hiyo kufungwa katikati ya wiki hii kwenye kombe la Europa, Naye mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo bwana Edwood, taarifa zinaeleza kuwa ameweka tayari mipango yake ya kumfukuza kocha wa timu hiyo Louis Van Gaal endapo atapoteza mechi ya Jumatatu dhidi ya Shrewsbury kwenye kombe la FA.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment