Hiddink; Ataoa sababu ya kumtoa Hazard.

Eden Hazard.
Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Guus Hiddink akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mchezo wao wa jana dhidi ya mabingwa wa Ligue 1 Paris Saint Germain (PSG) aligusia vitu kadhaa kimojawapo kikiwa ni kumtoa mshambuliaji wa klabu hiyo Eden Hazard. Hazard alitolewa katika dakika ya 70 ya mchezo na kocha wake huyo ameeleza kuwa mpaka kufikia dakika ile ya mchezo Hazard hakuwa na madhara tena kama ilivyokuwa katika dakika za mwanzo na ndipo alipoamua kumuingiza Oscar kuchukua nafasi yake, Pia Hiddink amemuonya Hazard kuwa kama anataka kurudi kwenye kiwango chake na ajihakikishie namba katika kikosi hicho ni lazima afanye mazoezi kwa bidii sana. Mechi ya jana ilikuwa ni mechi ya nne kwa Hazard kuanza chini ya kocha huyo na ya tisa huku akikosa mechi tatu kutokana na majeruhi.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment