Giroud; Tutaifanya Barcelona kama tulivyowafanya hawa.

Olivier Giroud.
Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud amewatambia Barcelona na kuwaambia kuwa watafanya kila wawezalo kuwasimamisha kwenye mchezo wa leo. Giroud akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema tulicheza na Bayern wakiwa hawajafungwa na timu yoyote ulaya lakini sisi tuliwafunga bila shida, jambo lile linatupa nguvu sana kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya timu hii nzuri ya Barcelona na tunaamini tutafanya kama tulivyofanya dhidi ya Bayern tena kwa ubora zaidi. Arsenal leo watapambana na klabu ya Barcelona kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa ulaya kwenye dimba la Emirates muda wa saa nne na dakika arobaini na tano.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment